Friday, August 21, 2009

KAZI ILIANZA HIVI MDAU!!!Zilikuwa mbio za kufa mtu.
Ukatumika ujanja wa mchezo wa soka,unaona bwana!!!!Analazimishwa kuelekea ulipo mtego.
Hatimaye akaona humu ndio salama yake,kumbe!!


Baada ya mbio za umbali kadhaa hatimaye yebo yebo imefanya kazi yake.


Amepatikana sasa kinachofuta ni.......


Wengine wamekamatwa kwa mtindo kama huu wamehifadhiwa kwenye kiroba.

Wako machinjioni sasa.

Miguu pamoja na mikia inatenganishwa kwa kutumia kisu chenye ukali wa kutosha tu.

Mkia huo unakatwa mdau.

Mikia ya kenge hao ikiwa katika sahani
Ameshachunwa ngozi sasa hivi ndivyo anavyoonekana.

Kenge hao wakiwa tayari wameshachunwa ngozi kama wanavyoonekana mdau.
Kazi ya kuwakata kata imeanza ambapo unaandaliwa msosi wa mchana mdau.

Chakula kipo tayari kwaajili ya kuliwa mdau.
Hii ndiyo biriyani ya kenge mdau,unaonaje?
Karibu kula tuliliwaze tumbo mdau.....

3 comments:

 1. Mambo yenyewe ndo kama haya basi kuanzia leo naacha kula nyama. Mimi na matembele pia kisamvu bila kusahau mboga za maboga.

  ReplyDelete
 2. Unagiza tuuu hotelini, kisha unasifia ladha ya "nyama za huku" bila kujua huku ni wapi na kwao nyama ni nini. Lol
  Mwendo wa majani majani tuuu. Nyama si afya

  ReplyDelete
 3. That was the most disgusting meal i ever saw,can't belive ppl eat that?!!lol

  ReplyDelete