Tuesday, June 4, 2013

ULIVYOKUWA UNAKUNYWA HUKUJUA KAMA ZITAKUFANYA HIVYO???


Anayejiita Dj na msanii mkoani Iringa amezima baada ya kupiga ulabu wa kutosha tu wakati wa uzinduzi wa klabu ya La Parte mwishoni mwa wiki.

NIMEFANYA KILA NALOTAKA KATIKA UJANA WANGU SASA NIMEAMUA KUTULIA NA HUYU!!.Bondia Amir Khan akiwa na mke wake Faryal Makhdoom..Amir Khan 26 mwishoni mwa wiki iliyopita amefunga ndoa na Faryal Makhdoom katika sherehe ya kimila iliyofanyika katika hoteli ya Waldolf Astoria huko jijini New York.

Maharusi hao walionekana wakiwa katika mavazi ya kiutamaduni ya Kihindi ambapo bondia huyo aliahidi kuachana na maisha ya matanuzi na kutenga muda wa kutosha kwa mke wake ambae ni mwanafunzi wa political science.

Bondia huyo ameliambia jarida la Hello ameishi maisha ya ujana,amefanya kila kitu alichokuwa anakitaka kukifanya lakini sasa ameamua kutulia na kuamua kuwa na familia yake.

Khan amesema kuwa baada ya kufunya sherehe hiyo ya dini ya kiislam iliyofanyika huko Marekani,ametaka marafiki zake wanaoishi Uingereza kukaa tayari kwa pati kubwa itakayofanyika huko wiki ijayo.

Thursday, May 30, 2013

ADRIAN MUTTU ATAKA KUMUASILI MTOTO ALIYETUPWA CHOONI HUKO CHINA....


Mchezaji wa zamani wa Chelsean Adrian Muttu


Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Uingereza Chelsea Adrian Mutu ameeleza nia yakwe ya kumuasili mtoto aliyenusurika kufa kimiujiza baada ya kutupwa chooni huko nchini China.
Mtoto huyo aliokolewa na waokoaji katika mji wa Jinhua uliopo katika  jimbo la mashariki la Zhejiang nchini china baada kukatwa kwa bomba la maji taka aliponasa baada ya kutupwa na mama yake baada ya kujaribu kujifungua kwa siri.
Habari za kutupwa kwa mtoto huyo zilisambaa kwa haraka duniani kote baada ya kutolewa kwa picha za video zilizowaonesha waokoaji na watumishi wa kikosi cha zima moto walipokuwa katika jitihada za kumuokoa mtoto huyo kwa kujaribu kukata bomba lenye ukubwa wa kipenyo cha sentimita 10 kwa kutumia mamba(pliers) na misumeno.

Baada ya kusambaa kwa kasi kwa taarifa za mtoto huyo hatimaye mapema hii leo amejitokeza Adrian Mutu mcheza soka wa zamani wa klabu ya Chelsea aliyejiunga na timu hiyo kwa dau la paundi milioni 15.8 mwaka 2003 kabla hajatimuliwa klabuni hapo baada ya kushindwa kufanyiwa vipimo alivyokuwa afanyiwe ili kuthibitisha kama hatumii madawa ya kuongeza nguvu.
Mchezaji huyo raia wa Romanian amekiambia kituo kimoja cha televisheni nchini mwake cha channel ProTV nia yake ya kumuasilia mtoto huyo.


Mutu baba wa watoto watatu amesema kwa sasa yuko katika majadiliano na mke wake Consuelo ili kuona ni namna gani wanaweza kuwasiliana na wazazi halali wa mtoto huyo ili waweze kuingia makubaliano ya kisheria yatakayowawezesha kumuasili mtoto huyu.

Licha ya nia nzuri ya mchezaji huyo anaeichezea klabu ya AC Ajaccio ya Corsica kutaka kumuasili mtoto huyo huenda akakumbana na vikwazo baada ya nchi yake ya Romania kutokuwemo katika listi za nchi 17 ambazo haziwezi kuasili watoto kutoka nchini China.

Mutu,34 amekiambia kituo cha televisheni cha channel ProTV kuwa baada ya kuiona video hiyo hakuona sababu za kuendelea kuishi na kufurahia kifungua kinywa kila asubuhi kwa kuwa mtoto huyo ni shujaa na atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake ili kumuasilia mtoto huyo kwa kuwa anaamini ameletwa kwake na mungu.


Akitolewa kutoka katika bomba la maji taka


Amesema awali hakuwahi kufikiria kuasili mtoto lakini kwa tukio la mtoto huyo ameguswa na kudai kwamba lazima amsaidie.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini China mtoto huyo ametambuliwa kutokana na namba yake aliyopewa hospitali na alifikishwa hospitalini hapo akiwa na mapigo ya moyo ya chini kabisa huku mwili wake ukiwa na michubuko na majeraha madogo madogo lakini hali yake imetengemaa kwa sasa.
Mama wa mtoto huyo ameeleza kujutia kitendo chake cha kumtupa mtoto wake katika mfumo maji taka na kusisitiza kuwa hakumtupa kwa makusudi isipokuwa alijifungua ghafla baada ya kuumwa tumbo na kukimbilia msalani kwa lengo la kujisaidia.

Mama huyo mwenye miaka 22 amewaambia polisi kuwa mtoto wake huyo aliyezaliwa akiwa na kilo 5 alitumbukia katika tundu la choo lililokuwa na upana wa nchi nne akiwa katika harakati za kuzuia damu iliyokuwa ikimtoka kwa wingi baada ya kujifungua.Akiwa hospitali anapatiwa matibabu


Hata hivyo polisi katika jimbo hilo la mashariki la Zhejiang wameviambia vyombo vya habari kuwa mama huyo alikuwa akijaribu kujifungua mtoto huyo kwa siri baada ya kushindwa katika jaribio lake la kuutoa ujauzito huo.


Mtoto huyo ameruhusiwa kutoka hospitali mapema hii leo asubuhi akiwa ana hali nzuri akiwa chini ya uangalizi wa wazazi wa binti huyo.


Katika hatua nyingine polisi katika mji huo wamefanikiwa kumpata mtu anayedhaniwa kuwa ni baba wa mtoto huyo ambae pia ametoa ombi la kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini kuwa ni mzazi wa mtoto huyo.