Wednesday, June 24, 2009

DOGO ANA NINI HUYU?


IKER CASILLAS amesisitiza kuwa Manchester United wasijisumbue kumshawishi kuondoka Real Madrid.

Kipa huyo raia wa Hispania amehusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na wazee hao wa Old Trafford katika majira ya joto.

Kuna taarifa zinasema kuwa boss wa United Alex Ferguson alikuwa tayari kutumia kiasi cha paundi milioni 80 atakazopata kama malipo ya Cristiano Ronaldo kwaajili ya kumpata Casillas.
Hata hivyo Casillas amekanusha kuwepo kwa taarifa hizo si kutoka kwa United wala klabu nyingine.

Ameongeza kuwa hata wakala wake na klabu yake bado haijapokea ofa yoyote mpaka sasa.

Ike anasema kuwa ana mkataba na Madrid hadi mwaka 2017 na kwasasa anafikiria kumaliza mkataba wake huo klabuni hapo.

"kila mtu anafahamu kwaba Madrid ipo moyoni mwangu na itaendelea kuwa hivyo mpaka kifo changu ”

"nilijiunga na Real Madrid nikiwa mdogo kabisa na hapa ni nyumbani kwangu ." alisikika kipa huyo katika moja ya mahojiano yake ya hivi karibuni kuhusiana na mustakabali wake wa soka.

No comments:

Post a Comment