Sunday, July 12, 2009

HATIMAYE LATOYA AZUNGUMZIA KIFO CHA KAKA YAKE.

Dada yake Michael Jackson La Toya usiku wa kuamkia leo amesisitiza kwamba kifo cha mfalme wa Pop kilipangwa kutokana na mali yake yenye thamani ya dola bilioni 1 katika inayotokana na muziki na kuongeza kuwa anawafahamu waliotekeleza mauaji hayo.

Akizungumza na gazeti la News of the world,La Toya mwenye umri wa miaka 53 amesema kifo hicho kilitokea ghafla ambapo mwili wa Michael ulikutwa na dawa nyingi mwilini na kiasi cha dola milioni 2 alizokuwa nazo pamoja na vito vyake vya thamani viliibiwa.

La Toya amesema hadhani kwamba mtu mmoja peke yake amehusika bali inaonekana wazi kwamba kulikuwa na mipango ya kupata fedha za Michael.

KATIKA MAHOJIANO HAYO LATOYA AMEBAINISHA MAMBO KADHAA YALIYOPELEKEA KIFO CHA KAKA YAKE.

Walimpa dawa nyingi.

Alikuwa peke yake na hakuwa anajiweza.

Hakutaka kufanya show jijini London.

Alilazimisha nyota huyo kufanyiwa uchunguzi wa pili.

Kiasi cha dola milioni 2 zilizokuwepo nyumbani kwake zimepotea.

Hata hivyo La Toya ameapa kuwashughulikia wauaji hao ambao hakutaka kuwataja na amesema atapumzika tu pale atakapowakamata .

La Toya amebainisha hayo siku mbili kupita baada ya mkuu wa polisi jijini Los Angeles kukiri kwamba wanaendelea na uchunguzi wa kifo cha Wacko Jacko.

La Toya ambaye inasemekana alikuwa karibu na Michael kuliko familia yake wote anaimani kuwa ndugu yake alizidishiwa dawa .

LATOYA HAKUISHIA HAPO AMEBAINISHA ZAIDI JINSI NDUGU YAKE ALIVYOFANYIWA NA WATU HAO.
Inasemekana wakati Michael anaaga dunia watu alikuwa amekaa nao walikaa na mwili wake kwa zaidi ya nusu saa.

Baada ya siku 17 kupita tangu afariki Michael,La Toya amejiuliza maswali mengi kuhusiana na mazingira ya kifo hicho.

Anasema kwamba Michael kwa muda alipewa dawa za maumivu ili aweze kujicotrol na aliwekwa mbali ili asikaribiwe wala kutembelewa na watu wake kwa maana ya familia yake.

Alifanyishwa mazoezi kwa muda mrefu yaliyomchosha na hakupenda kufanya zaidi ya show 50 kwa ajili ya maandalizi ya show ambayo ilitakiwa aifanye siku ya kesho jijini London.

kutokana na kuwa karibu sana na Michael, La Toya alichaguliwa na familia yake kusaini cheti cha kifo hivyo amesema huo ndio mwanzo wa uchunguzi wake na pia yeye(Latoya) ndiye aliyeamuru uchunguzi wa mara ya pili ufanyike.

Taarifaya uchunguzi huo inataraji kutolewa baada ya wiki mbili zijazo lakini tayari La Toya na wana familia wengine katika uchunguzi wao wameongeza kuwa kila mmoja atashangazwa na matokeo ya uchunguzi huo utakapotolewa.

AKIZUNGUMZIA MWILI WA NDUGU YAKE ULIVYOKUWA BAADA YA KIFO CHAKE LATOYA AMESEMA.......

Mwili wa Michael ulikuwa na matundu mengi ya sindano katika shingo yake na mikononi na mengi yatazungumzwa katika ripoti ya madaktari na kusitiza kwamba atahakikisha anawapata waliomua kaka yake hata kama ripoti hiyo itakuwa tofauti.

Dada huyo amebainisha wazi kwamba miaka michache iliyopita Michael aliwahi kumwambia kuwa kuna watu wanamfuatiliwa na wataka kumuua kutokana na uwezo wake wa kujitangaza pamoja na vifaa na hata yeye alikuwa na wasiwasi na maisha ya ndugu yake baada ya kuelezwa hivyo.

Amesema kwa sasa hataki kuharibu ushahidi wa polisi lakini ni ukweli kwamba Michael aliwindwa kwa muda na aliishi na watu ambao walikuwa na nia ya moyo wake na yeye kama dada alihisi kwamba huenda kuwa ndugu yake huyo angeuwawa kabla ya show yake iliyotakiwa kufanyika kuanzia kesho jijini London.

La Toya anasema siku za mwisho yeye na hata wanafamilia wengine walizuiwa na watu wake kutomuona na akibainisha kuwa hata baba yake alijaribu mara kadhaa kuonana nae lakini ilishindikana.

Anadai kwamba watu hawa ambao hajawataja majina walijaribu kadri wawezavyo kumfanya Michael awe mkiwa hali ambayo ingepelekea kuchoka kiakili ili ajihisi kuwa mtu mpweke kuliko wote duniani .

Na kweli watu hao wamefanikiwa huku akitoa mfano kwamba ukitaka kumtawala mtu basi mtenge au ukitaka kutawala watu basi wagawe.

Kuhusu fedha zilizoibiwa La Toya amesema fedha hizo ziliibiwa siku aliyokufa pamoja na vito vyenye thamani huku akiongeza kuwa kawaida Michael alikuwa anapenda kuwa na fedha taslim ndani ya nyumba kiasi cha dola milioni 2 .

La Toya amesema watu wengi walizungumza kwamba Michael hakuwa tajiri lakini ukweli ni kuwa alikuwa na fedha taslim kila mara.

No comments:

Post a Comment