Saturday, July 18, 2009

MENGI YAZIDI KUIBUKA BAADA YA KIFO CHA MICHAEL JACKSON.

Rafiki wa zamani wa Michael Jackson ambaye pia alikuwa mtaalamu wa ngozi Arnold Klein ameibuka na kusema kuwa mfalme huyo wa muziki wa Pop ulimwenguni hakuwa na uwezo wa kuzaa kutokana na kujeruhiwa mara mbili korodani zake.

Katika mahojiano yaliyorekodiwa na mtandao mmoja wa nchini Marekani, Paul Gohranson – ambaye ni mtaalamu wa kuchua misuli na aliyewahi kuishi kimapenzi na Klein amesema kuwa Jacko alipoteza uwezo wake wa kutengeneza mbegu za uzazi baada ya baba yake kumpiga korodani zake.

Gohranson aneleza kwamba hali hiyo ndiyo iliyopelekea patna wake wake wa zamani kujitolea mbegu zake ili kumwezesha Jacko kuwa baba.

Amenukuliwa akiimuuliza "Arnold kwanini Michael Jackson asitumie mbegu zake mwenyewe? alijibiwa kuwa Michael alikuwa hawezi kuzaa."

Akifafanua Arnold alisema kuwa Klein alimwambia na kumthibitishia mara mbili kuwa Michael Jackson aliwahi kumwambia kuwa alipigwa sehemu zake za siri mara mbili kwanza wakatia akiwa mtoto mdogo ambapo baba yake alimnyanyua mguu wake mmoja na kuanza kumpiga.

Anasema kuwa Klein aliendelea kumueleza kuwa baba yake Michael hakudhamiria jkumpiga sehemu zake hizo za siri wakati huo lakini ndiyo hivyo imetokea na ilimsababishia maumivu makali sana Michael.

Mara ya pili ilikuwa pale Michael alipotoa albamu yap eke yake na haikufanya na kila mtu alimjia juu Jacko kuwa anapoteza sauti yake,anapoteza mtazamo wake na huenda akaitia aibu familia ya Jackson.

Jamaa akiendelea kusimulia mkasa huo anasema baada ya Michael kumaliza kumwambi yote hayo machozi yalikuwa yakimtoka na haya yote alikuwa akieleza baa ya kufanyiwa vitendo hivyo alisema Klein.

Hata hivyo baba yake Michael Joe Jackson, 79 kati kati ya juma hili amekanusha kwamba aliwahi kupiga mtoto wake huyo kiasi hicho wakati wa utoto wake.

Familia ya Michael kwa uda mrefu ilikuwa ikilalamikiwa kwa ukatili dhidi ya mwanamuziki huyo hasa katika kipindi ambacho ilikuwa ikisimamia kazi za Jackson 5.

Katika utetezi wake mzee Joe amewahi kusikika akisema kuwa hakuwahi kuwa fanyia vitendo vya kikatili watoto wake hao wakoseapo.

1 comment:

  1. Karibu Allen hivi ndivyo vijiji vya watu wa kufikirika na kusadikika kwa yale yaliyojiri,yanayojiri na yale yatakayojiri, ukibarizi katika vijiji hivi kwa wema hakuna atakayekubughudhi, utatembelea mtoni, nyikani,jangwani na hata baharini ili mradi huvunji heshima za watu, huku kuna uhuru mpana kuliko huko uliko ilimradi ni wewe mwenyewe kujihesshimu na kulinda heshima yako na watu watakulinda pia, wapo wanaoweza kukudhihaki kwa kutumia majina ya kificho na wapo watakaotumia majina ya kughushi ilimradi kila mtu na mtazamo wake, usitumie uga huu kufanya malumbano na watu yanaweza kukukuta yasiyostahili kukukuta ilhali u kijana unayetarajia kuwa baba wa fulani punde ukamwacha mwanao anahangaika kutokana na wewe kuwa nguvuni kwa kuchonganisha jamii kwa hili GAZETI TANDO,wapo walitangulia jenga desturi ya kuwatembelea vijiji vya wenzio ili nao wakutembelee utajifunza mengi.

    Ni haya tu!!!! karibu sana naona wanyalu wamekufanya usahau washikaji wako!!!lakini kijiji chako kizuri kinapendeza sanaa!!!

    ReplyDelete