Saturday, July 4, 2009

TWAKUTAKIA KILA LA KHERI KAKA!!!


RED HOT …Michael Owen hatimaye amekamilisha ndoto yake ya kuhamia Manchester United baada ya kupita katika majaribio ya afya.

Owen amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Manchester United licha ya mashabiki wa timu hiyo kutoa maoni yao kwenye mitandao ya internet wakihoji kusajiliwa kwa mchezaji huyo majeruhi aliyewahi kuichezea klabu ya Liverpool.

Hata hivyo mshambuliaji huyo ameahidi kuanza ligi msimu ujao kwa kishindo na kusema kuwa Alex Ferguson hakukosea kumjumuisha katika kikosi chake.

Akizungumza na wanahabari Owen amenukuliwa akisema "Nafahamu kuna watu wanamlaumu Fergie kwa uamuzi wake wa kunisajili lakini minong’ono hii itafikia tamati tamati katika mchezo wa kwanza nikiwa dimbani hapo nitaongea kivitendo zaidi."

Owen mwenye umri wa miaka 29 amefanikiwa kucheza zaidi ya michezo 500 akiwa katika kiwango cha juu katika klabu na hata timu ya taifa ya Uingereza.

Akizungumzia uhamisho huo Owen amesema kuwa ilikuwa kama ndoto baada ya Hull City kuwa timu pekee iliyokuwa ikimuhitaji lakini mambo yalibadilika baada ya mchezaji kupokea simu kutoka kwa kocha wa Manchester united Ferguson mapema jumatano ya juma hili.

No comments:

Post a Comment