Saturday, July 4, 2009

WAHUSIKA HAMUONI KAMA LIMEJAA???


Majuma kadhaa sasa yamepita toka mji wa Iringa upate nafasi ya pili kitaifa kwa kuwa miongoni mwa miji safi hapa nchini lakini hali ni tofauti katika baadhi ya maeneo mkoani hapa.

Hali ambayo inazua utata vigezo gani hutumika kutoa ushindi huo,hapa ni eneo la soko kuu la mkoa wa Iringa ambapo hali ya usafi kikweli si nzuri kama unavyojionea jidude hilo likiwa limejaa uchafu huku wahusika wakiangalia kama haliwahusu vile!!!!

Wahusika wa usafi Manispaa ya Iringa msilewe na hizo sifa zindukeni toka usingizini tembeleeni maeneo yenu ya kazi.

1 comment:

  1. Ningependa kujua mji wa mwisho ulikuwa upi kisha tumuombe "mwanajamvi" mmoja aende kutufotolea taswira za huko tujionee. Maana kama mji msafi ni hivi, basi huo mchafu lazima utakuwa ni "Dampo city"
    Bless

    ReplyDelete