Saturday, August 29, 2009

FINAL WHISTLE!!



United wameshinda kwa jumla ya magoli 2-1 hii ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Arsenal kushindwa katika msimu huu huku Man wakiwa tayari wamekwishaonja chungu ya kufungwa baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Burnley.

Mambo mengine yalikuwa ni hivi dakika ya 95 Wenger alipewa adhabu ya kutolewa nje ya uwanja na mwamuzi wa nne.

Dakika ya 94 Van Persie alibahatika kuichambua ngome ya United lakini bahati haikuwa yao kwani tayari Gallas alikuwa amekwisha otea.

Najua mtaa wa pili kulala itakuwa ishu.usiku mwema mdau.

No comments:

Post a Comment