Wednesday, August 26, 2009

HII NDIO HALI HALISI ILIVYOKUWA IDODI.



Hii ni njia ya kuelekea Idodi kunako shule ya sekondari Idodi,na hata ile mbuga yenye umaarufu Afrika na hata duniani kote Ruaha National Park,barabara imejengwa kwa kiwango cha changarawe.

Naomba nikiri hapa hali barabara ni nzuri kiasi japokuwa muwezeshaji hapo chini alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya barabara hii,sifahamu wakati wa mvua hali ya barabara hii inakuwaje?tuombe uhai mvua zikianza nitafanya tena ziara huku.



Ilikuwa ni safari ya kuelekea Idodi sekondari nikiambatana na baadhi ya wadau wa Ebony Fm kwaajili ya kupata undani wa hili na lile kuhusiana na tukio la kupoteza maisha kwa baadhi ya wanafunzi wasichana wa shule ya sekondari hiyo baada ya kuteketea kwa moto.



Mabaki ya vitu mbali mbali vilivyokuwemo katika bweni la wasichana la sekondari ya Idodi.



Hii korido ya bweni la wasicha la shule ya seokondari Idodi lililoteketea kwa moto,kama inavyoonekana mdau,Pia nilikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika eneo hilo kutoa heshima zetu za mwisho kwa wanafunzi hao wapatao kumi na wawili.



Huu ni mlango wa kuingilia chumba ambacho baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi,Iringa wanaelezwa kufa baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.



Baadhi ya mabaki ya vitu kama madaftari,mabegi ya wanafunzi waliopoteza uhai wao katika chumba hiki kutokana na ajali ya moto.



Hapa ndipo ndoto za kimaisha za wapendwa wetu waliokuwa wakitafuta mkate wa watoto hapo baadaye zilipokatika.



Hapa ni ndani ya chumba ambacho kinaelezwa kuwa kilikutwa kikiwa na miili ya baadhi ya wanafunzi ikiwa imeteketea kwa moto hali iliyopelekea kutotambulika kirahisi.



Kila kitu kiliteketea hapa kwa moto mdau.



Hii ni sehemu ya nyuma ya bweni la wasichana la shule ya sekondari Idodi lililoteketea kwa moto.



Sehemu ya dirisha la bweni la wasichana la shule ya sekondari Idodi liloteketea kwa moto juma lililopita.



Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,akifuatiwa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Jumanne Maghembe na mkuu wa mkoa wa Iringa Mohammed Abdulaziz wakiwa katika eneo la shule ya sekondari Idodi kuhudhuria maziko ya wanafunzi waliofakufa kutoka na ajali ya moto.



Baadhi ya viongozi wa chama na serikali waliohudhuria maziko ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi.



Shehe wa dini ya kiislam akifanya ibada ya kuiombea miili ya wanafunzi kumi na wawili wa shule ya sekondari Idodi.



Viongozi wa dini ya kikatoliki wakiendesha misa ya kuiaga miili ya wanafunzi kumi na wawili wa shule ya sekondari Idodi mkoani Iringa waliokufa katika ajali ya moto ulioteketeza bweni la wasichana shuleni hapo.



Majeneza 12 ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi waliokufa kwa ajali ya moto yakiwa yamepangwa tayari maziko.

Kinachosubiriwa hapa ni kuushusha kaburini mwili wa marehemu huyu ambaye bado hafahamiki jina lake ni nani kutokana na kuungua kwa na hivyo kupelekea kutotambulika kwa urahisi.
Tayari mwili wa mmoja ya wanafunzi ukiwa umeshushwa katika kaburi baada ya taratibu zote za mazishi kukamilika,Mwenyezi mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu amen.

3 comments:

  1. Jamani inasikitisha sana nashindwa hata kuandika nini nilitaka kuandika. Wastarehe kwa amani. Na pole kwa wafiwa wote pia waIringa wote.

    ReplyDelete
  2. Yaani naona nilie tuu,,na mungu atuokowe kabisa hapa duniani kuna mambo mengi yanayotuumiza mpaka tunafika mbali sana ,,emungu walaze pema peponi...yoooh.

    ReplyDelete
  3. So sad..!may their soul rest in peace! AMEN

    ReplyDelete