Monday, August 24, 2009

HIKI NDIO KIPIGO ALICHOTOA STEVEN GERRARD!!


Huyu ndiye jamaa alieonja kipigo cha Steven Gerrard katika ugomvi uliotokea baa huko nchini Uingereza akionesha majeraha aliyoyapata kutokana na kibano hicho.

Marcus McGee, 34, alitapakaa damu mwili mzima hali iliompelekea awahishwe hospitali kupatiwa matibabu baada ya mkong’oto.

Jamaa ameeeleza kuwa kufuatia kipigo hicho aling’oka jino na kupata jeraha kichwani kama anavyoonekana katika picha baada ya kupigwa na glasi.

Hata hivyo baada ya kipigo hicho jamaa aliamua kufungua mashitaka dhidi ya Steven Gerrald lakini hata hivyo mchezaji huyo wa Liverpool alishinda kesi hiyo baada ya kuonekana kuwa alikuwa ajitetea.

No comments:

Post a Comment