Wednesday, August 12, 2009

USHUJAA UNAOTAFSIRIWA VIBAYA!!!!



Hili ni fuvu la kichwa cha chifu wa wahehe Mtwa Mkwawa au Mkwavinyika kama ambavyo walivyokuwa wakimuita wenyeji wa mji wa Iringa, kiongozi huyu wa kabila la Wahehe ambaye ngome yake ilikuwa katika mji wa Kalenga kilomita kadhaa kutoka mjini Iringa aliaumua kujiua kwa kujipiga risasi ili kuepuka kudhalilishwa au kukutwa hai na wakoloni wa Kijerumani.

Inaelezwa kuwa desturi hii ya kujiua au kujinyonga inaonesha ushujaa kwa wanaume na watu wengine wenyeji wa mkoa huu ikiwa ni ishara ya kukwepa kudhalilishwa kwa namna yoyote ile.

Lakini hii si desturi nzuri sana,lakini pia ni vyema ikakumbukwa kwamba Mkwawa alijiua ili kutetea ardhi ya nchi yake isivamiwe na wakoloni na si kwa sababu nyingine ambazo hazikutajwa.

Hivi baadhi ya wenyeji wa mkoa wa Iringa hutumia kigezo hicho cha kujiua ndivyo sivyo kwa kuamini kuwa wanapinga kuonewa ,kuudhiwa na Waume,Wake Wapenzi wao ama watu baki.

Habari hii ni kwa mujibu wa Rashid Mkwinda wa Fasihi za Ufasaha.

1 comment:

  1. Asante mdau kwa kuliweka wazi hilo,kwanini sijui watu hawaigi vitu vya msingi.
    badala yake wanafanya wanayoyajua wao kwa malengo wayajuayo wenyewe.

    ReplyDelete