Friday, August 14, 2009

WADAU HABARI NJEMA KWA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA!!Wadau naomba mpokee waraka huu wa utambulisho rasmi wa kampuni ya Mediakings Tanzania limited ikiongozwa na partners Godwin Gondwe na Patrick Gondwe.

Kampuni hii imejikita katika full multimedia production (Audio,Video na Graphics), pia katika matangazo ya redio mabango na kadhalika.

Ndani ya Media kings kuna studio mbili za Audio ambazo zinajulikana kama Music Laboratory kwa kifupi mLAB zikiongozwa na producer mahiri DUKETACHEZ (kama ulikuwa hufahamu huyu jama ndiye aliyetengeneza nyimbo kama Proffessional ya FID.Q, Traveller ya SOLO THANG na zero ya WITNESS wimbo ambao video yake ilishinda tuzo channel O)

Wadau kwa heshima na taadhima studio za mLAB inatambulisha toleo la kwanza kabisa la kazi zake kwa kuwa-Introduce wasanii wawili waliopo kwenye label hiyo ambao ni Nicky Mbishi – Punchline na Nendeze- boy

Nicky Mbishi ni mshindi wa pili wa mashindano freestyle yaliyofanyika pale coco beach yakiratibiwa na kipindi cha XXL cha clouds FM na pia ni msomi anaebukua katika chuo cha MTC-Mbeya akiwa mwaka wa pili.

Nendeze yeye ni msanii wa kike ambae hapo awali alikuwa akitumia jina la Tecla na alishawahikufanya tracks kadhaa hapo awali ingawa hazikuwahi kufika level ya kupewa shavu redioni.

Toleo la pili la kazi za mLAB itafakuwa ni tarehe 28 mwezi huu kwa kuwatoa wasanii wengine watatu ambao ni ROMA, Grace na Darlington.

Ndani ya mLAB pia kuna album kali inayopikwa ya msanii anaejulikana kama Musa vipaji vingi ambayo ina mahadhi ya kiafrika, ni album inayotarajiwa kufanya vizuri sana hasa ikizingatia jina la jamaa kama lilivyo.

Huyu jamaa yuko vizuri katika kupiga ala nyingi( instruments) na ni matunda na bado yupo na THT chini ya usimamizi wa Ruge Mutahaba.

Kwa wadau ambao mna ndugu na jamaa ambao ni wasanii na wanapenda kufanya kazi katika mlengo wa tofauti wasiliana na Mediakings Tanzania ltd na Music laboratory (mLAB) katika ofisi zao zinazopatikana maeneo ya Kinondoni Biafra jijini Dar es salaam (kumbukumbu street, opposite na YANNA tyre).

No comments:

Post a Comment