Monday, January 18, 2010

KUTANA NA FAMILIA ILIYOJIZATITI KUPAMBANA MAGAIDI!!


Tumejiandaa... Cameron, Katerina, Lee, Elijah, Emily, Megan, Morgana, Caleb na Raven wakiwa na baadhi ya silaha wanazozimiliki.

Familia hii imejiandaa kikamilifu kupambana na tishio lolote la ugaidi.

Msichana mdogo Morgana,mwenye umri wa miaka sita, ana uwezo wa kutumia silaha aina rifle yenye 22 calibre na anichukulia kama mdoli wa kuchezea.

Dada yake Raven,mwenye miaka tisa pia anayo silaha yake ambayo alinunuliwa na baba yake akiwa na umri wa miaka saba.Angali hapo chini mdau mtoto huyo kamkumbatia bunduki ina rangi ya pink.

Akijigamba binti huyo anasema baba yake baada ya kumnunulia bunduki hiyo alimwambia kuwa anaweza kuwa mlenga shabaha mzuri.

Baba wa familia hiyo Lee Miracle, wa kitongoji cha Sterling Heights, Michigan huko Marekani.anasema baada ya tukio la septemba 11 Lee,mke wake Katerina, 43 na watoto wao wenye umri wa kuanzia miaka sita hadi 17 wamejiandaa kukabiliana na mashambulizi kutoka kwa wavamizi wa kigeni.


Megan akiwa ameshika kwa umakini bastola yake anayimiliki.


Morgana(6) akiwa na bunduki yake.


Megan akiwa tayari kukabiliana na adui kwa kutumia bunduki yake.

FamilIA hiyo wakiwa katika mapumziko na silaha zao kama kawaida.
Nimwagie maoni yako hapa chini mdau.....

3 comments:

  1. du mdau sasa hili balaa gani tena! kaaz kwel kwel

    ReplyDelete
  2. Dhahma likitokea hapo hawa wote wanaingia chini ya uvungu hakuna hata mmoja atakayekumbuka kuchukua bunduki

    ReplyDelete