Wednesday, July 6, 2011

AMIR KHAN KUZICHAPA NA MAYWEATHER.


Bondia Amir Khan anaetarajia kuzichapa na Mayweather.

Kambi ya bondia wa Uingereza Amir Khan imemuandalia mapambano manne bondia wao ikiwa ni maandalizi kabla ya kukutana Floyd Mayweather Jnr.

Habari kutoka kambi ya Mayweather zinasema bondia huyo amekubali kitita cha dola za kimarekani milioni 100 ili aweze kuzichapa na Khan katika majira ya joto mwaka ujao.

Pambano hilo katika wakati muafaka ambapo mabondia wote wawili wanashikilia rekodi nzuri ya kutokupoteza mapambano yao ya awali.


Mayweather akifafanua jambo mbele ya wanahabari.

Habari hizo za Khan kuzichapa na Mayweather zimewekwa bayana huko jijini London na Richard Schaefer,ambae ni mkurugenzi mtendaji wa Golden Boy Promotions ya nchini Uingereza.

Kabla ya pambano hilo dhidi ya Mayweather,Khan atakutana na bondia Zab Judah huko Las Vegas Julai 23 mwaka huu na baada ya hapo anatarajiwa kupigana na bondia kutoka Mexico Erik Morales.

Baada ya mapambano hayo Khan ataingia kambini kujiandaa kwa pambano lake na Mayweather bondia anayetajwa kuwa na changamoto nyingi awapo ulingoni.

1 comment:

  1. Sijui kwanini sina uhakika na uwezo wa Mayweather baada ya muda wote huu ambao kimtazamo wangu anapigana kimaneno zaidi tokea aritaye kipindi ile!:-(

    ReplyDelete