Friday, December 21, 2012

Coming from America: Golden Boy wapania kuwekeza Uingereza.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Golden Boy,Richard Schaefer.

Kampuni ya kupromoti mchezo wa ngumi inayofanya vizuri kwa sasa nchini Marekani Golden Boy ina mipango ya kupanua shughuili zake za kukuza mchezo wa ngumi kwa kuwekeza nchini Uingereza.

Kampuni hiyo ambayo inamdhamini bondia Amir Khan,imedhamiria kuingia mkataba na baadhi ya mabondia wa Uingereza walioiwakilisha nchi yao katika michezo ya  Olimpiki iliyofanyika jijini London mapema mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Golden Boy,Richard Schaefer amenukuliwa hivi karibuni akisema wamejipanga kuingia mkataba na mabondia hao na haijalishi kama walipata medali ama walikosa.
|
Amesema lengo la kampuni yake ni kupata mabondia wazuri kutoka Uingereza wenye vipaji na uwezo wa kupigana kama ambavyo walifanya wakati wakiiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki.

Bosi huyo wa Golden Boy ameweka bayana kuwa atatumia kiasi kikubwa cha muda wake nchini humo kusaka mabondia hao na kuwang’arisha katika ulimwengu wa ngumi na kuongeza kuwa hiyo ni mara yake kwanza kufanya hivyo toka aingie katika kupromoti ngumi.

Aidha bosi huyo amesema kwamba baada ya mabondia hao kupatikana wataandaliwa mapambano manne nchini Uingereza na Marekani pia na mapambano ya kwanza yatafanyika Uingereza katikati ya mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment