Tuesday, December 25, 2012

SOMO LA CHRISTMAS KWA WANANDOA MLIOTENGANA...


Heidi Klum na Seal katika picha ya pamoja(wakati huo)ambapo kwa sasa inaripotiwa wataweka tofauti zao pembeni kwa muda na kusherekea sikukuu ya Christmas na watoto wao.
Heidi Klum na Mtalaka wake Seal huenda wakaungana wakati wa sikukuu ya Christmas na kuweka tofauti zao pembeni kwa muda na kusherekea sikukuu ya Christmas pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari wazazi wenza hao wamefikia muafaka huo kwaajili ya kuweza kupata muda wa kuwa pamoja na watoto wao Leni, Henry, Johan na Lou.

Uamuzi wa Heidi na Seal kuungana na kusahau tofauti zao kwa muda kwaajili ya watoto wao ni  wa kuigwa kwani ni wachache sana tunaweza kufikia maamuzi haya mazito hasa baada ya kutengana na wake au waume zetu.

Wengi wetu hasa baadhi ya Watanzania tumekuwa na kasumba ya kuziacha familia zetu katika nyakati kama hizi na kwenda kujumuika na watu baki pasipo kutambua thamani na umuhimu wa familia zetu.

Wakati huu wa sikukuu ya Christmas ni wakati ambao familia huungana pamoja kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kula,kunywa na kupeana zawadi hasa kwa watoto,kwa hivyo tusitumie nafasi hii kwa kufanya mambo yatakayo ziumiza familia zetu kwa namna moja au nyingine.

Nakutakia Heri ya Christmas na Mwaka Mpya.

2 comments:

 1. It's going to be ending of mine day, however before finish I am reading this great post to increase my knowledge.
  my webpage :: OnlyCruiser.com

  ReplyDelete
 2. Come forward to us & get solution for your income problems ,(11548)
  Complete Our 3 day work at home training course and be
  placed in a work at home job, with a real company that
  will earn you over $50,000 per year Guaranteed!
  Earn up to $100,000 Per year from home
  as a certified home worker for more details visit: (http://www.JobzInn.com)

  ReplyDelete