Wednesday, December 19, 2012

TIMU YA MAKAPELA EBONY FM YAZIDI KUPUNGUA MAKALI....

Twalib Omary mtangazaji wa Ebony Fm,Iringa akifungishwa ndoa na Sheikh Seleman Makanjira katika  Msikiti wa Muuminin Kiwalani kwa Gude jijini Dar es salaam wakati akimuoa Bi Fatma Juma na baadae shughuli kufanyika Temeke Sandari nyumbani kwa Mzee Muwa.
       
                                   Huyu ndio Bi.Fatma Juma mke wa Twalibu Omary.

Twalibu hakuwa peke yake huku alisindikiza na baadhi ya wafanyakazi wenzake kutoka Ebony Fm kama  wanavyoonekana kuanzia kushoto ni Brother Dossi Magambo na upande wa kulia kabisa ni Yahaya Mohamedy.
 Msafara kuelekea Temeke nyumbani kwa Mzee Muwa kwaajili ya Tafrija fupi.

 Bwana kapata Bibi na Bibi kapata bwana wenye chuki jinyongeni,Twalib na mkewe Fatma wakijipa raha.

Baadhi ya marafiki wa karibu wa Twalib Omary kutoka Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na shemeji yao.


Twalib akiwasili nyumbani kwa Mzee Muwa akiwa na mkewe Fatma,kushoto kabisa (Mbele)ni mama mzazi wa bwana harusi.

 Karibuni nyumbani maharusi........

Bosi wa kipindi cha Anga la Michezo,Ebony Fm akimsindikiza mkewe kwenye gari baada ya tafrija fupi nyumbani kwa Mzee Muwa.

 Bosi huyoooo ameoa.......


 Mmiliki wa blog ya Kiujamaa Zaidi Yahaya Mohammedy Kulia akiwa katika picha ya pamoja na maharusi.

Picha zote hizi ni kwa hisani ya www.kiujamaazaidi.blogspot.com ambayo ilishuhudia tukio hilo la kufungwa ndoa kati ya Twalib Omary na Fatma Juma huko jijini Dar es salaam tarehe 16/12/2012.

1 comment: