Tuesday, June 9, 2009

HATIMAYE AZUNGUMZIA YALIYOWAHI KUMSIBU!!!


Hatimaye kwa mara ya kwanza rapa machachali ulimwenguni Queen Latifah amezungumza kuwa ameshawahi kufanyiwa vitendo vya uzalilishaji wa kimapenzi wakati wa utotoni.

Akizungumza na na jarida la Essence mwanamuziki huyo amesema alikuwa akifanyiwa hayo na yaya(mlezi wa watoto) hali iliyomfanya ashindwe kuwa na mahusiano na watu walionesha nia ya kuwa na mahusiano nae alivyokuwa mtu mzima.

Latifah, 39 ameongeza kwa kusema yaya huyo alimnyanya sana na hakumwambia mtu yoyote kuhusiana na matukio hayo.
Anasema alificha siri hiyo ndani kabisa ya moyo wake na hakutaka kabisa mtu yeyote kumsogelea karibu.
Akifafanua anasema tukio hilo lilimfanya mambo yake mengi kuchelewa vinginevyo angekuwa ameolewa miaka mingi iliyopita.

No comments:

Post a Comment