Wednesday, June 10, 2009

MIKE TYSON AOA WIKI MBILI BAADA YA KUFIWA NA BINTI YAKE!!!

Bingwa wa zamani wa ndondi Mike Iron Tyson ameoa kwa mara ya tatu,wiki mbili baada ya kufiwa na mtoto wake katika ajali ya kusikitisha.

Bondia huyo wa uzito wa juu alionekana akiwa na mke wake mpya Lakiha Spicer huko mjini Las Vegas baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa la Las Vegas Chapel.

Kwa mujibu wa mmiliki wa kanisa hilo Shawn Absher ndoa hiyo ilifungwa kanisani hapo jumamosi iliyopita. Rekodi za ndoa zinazofungwa katika mji wa Las Vegas zinaonesha kuwa Tyson (42) alipata kibali cha kumuoa Spicer (32) nusu saa kabla ya sherehe yao.

Absher amesema kuwa bingwa huyo wa zamani wa masumbwi na mkewe mpya walitaka sherehe yao iwe ya kawaida tu bila kuwa na mlolongo wa vitu vingi.

Tyson,ambaye amepewa shavu katika ucheshi mpya unaokwenda kwa jina la The Hangover,kabla aliwahi kufunga ndoa na mcheza filamu Robin Givens mwaka 1988 na baadaye Monica Turner mwaka 1997.

Ndoa yake ya kwanza ilivunjika mwaka mmoja baada ya Givens kudai talaka baada ya kudai kuwa alikuwa akimuogopa mumewe Tyson, wakati ndoa yake na Turner ilidumu kwa miaka mitano.

Pichani ni Mike Tyson na mkewe mpya Lakiha Spicer,picha hii ilipigwa mwaka 2008.

Hapa bingwa wa zamani wa masumbwi ulimwenguni akiwa amembeba mtoto anayeaminika kuwa Exodus,ambaye alifariki wiki mbili zilizopita.

Mwezi uliopita mtoto wa bingwa huyo wa zamani wa masumbwi alifariki dunia baada ya kujinyonga kwa bahati.

Mtoto huyo wa Tyson alikutwa akining’inia nyumbani kwa bingwa huyo katika mji wa Phoenix, Arizona,mtoto huyo alikutwa na kaka yake Miguel, ambaye alimwita mama yake ambaye alikuwa akifanya usafi pembezoni mwa nyumba yake.

Tyson baada ya tukio hilo alitoa tamko kwamba hana neno la kuzungumza kufuatia tukio hilo la kufiwa na binti yake.

Hapa Tyson akiwa katika baadhi ya sehemu alizoigiz katika ucheshi mpya unaoitwa The Hangover,ambao simulizi yake inawahusu mabachelor.

1 comment:

  1. INGEKUWA BONGO TUNGESEMA UNAJIONGEZEA MIZIGI.

    TUNAFAHAMU UMEFULIA HILO HALINA UBISHI.

    ReplyDelete