Monday, August 17, 2009

HATIMAYE ZOMBE NA WENZAKE WAACHIWA HURU.Mahamaka kuu jijini Dar es Salaam imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar es Salaam Abdallah Zombe na wenzake baada ya kukutwa hawana hatia ya kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara ya madini.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Kiongozi Salum Massati baada ya mahakama hiyo kuchambua ushahidi wa upande mashtaka na ule wa utetezi uliokuwa na mashahidi 37.

Akuzungumza kwa njia ya simu wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwepo mahakamani hapo wakati hukumu hiyo ikitolewa.

Amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo haumuoneshi mshitakiwa hata mmoja kuwa anahusika na mauaji hayo badala yake unamtaja mtuhumiwa mwingine anayetajwa kwa jina la koplo Sadi.

Amesema ushahidi huo unawaunganisha washitakiwa walioachiwa huru jioni ya leo,lakini kwa kuzingatia kuwa mtu anyesadikika kuwa anahusika na mauaji hayo hakuwepo mahakamani kwa hivyo washitakiwa waliosalia hawawezi kupatikana na hatia.

Hata hivyo mpaka hukumu hiyo inatolewa haikuweza kufahamika mahali alipo Koplo Sadi lakini mashahidi wote na baadhi washitakiwa walionesha kuwa walikwenda katika eneo la msitu wa pande uliopo mbezi Luis jijini Dare s salaam ambapo wanamtaja koplo Sadi kuhusika na mauaji hayo.

Taarifa kutoka mahakamani hapo zimeleeza kuwa kesi hiyo imehudhuriwa na umati mkubwa wa watu hali ambayo imeifanya mahakama hiyo kuamuru baadhi ya watu kutoka nje na kusikiliza kesi hiyo kupitia vipaza sauti.

Mkuu huyo wa zamani wa upelelezi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam na wenzake walikuwa wanatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge Mkoani Morogoro na dereva taxi mnamo January 14 mwaka 2006 kwenye msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis jijini Dar es salaam.

Kesi hiyo ilianza mwaka 2006 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, kesi hiyo ilihamishiwa mahakama kuu.

2 comments:

  1. Aaaaaaaaawapi bado wanatuletea uhuni hawa watu mazeeeee wanatuona watanzania ni wajinga hatuelewieeh? watuhumiwa wote vigogo wanaachiwa, STILL NO JUSTICE IN TANZANIA UNTIL WHEN???????

    ReplyDelete
  2. Aaaaaaaaawapi bado wanatuletea uhuni hawa watu mazeeeee wanatuona watanzania ni wajinga hatuelewieeh? watuhumiwa wote vigogo wanaachiwa, STILL NO JUSTICE IN TANZANIA UNTIL WHEN???????

    ReplyDelete